AFISA MAZINGIRA II (19 Posts)

Job Description

  1. Kutekeleza programu za mara kwa mara na maalum za kuhamasisha uzingatiaji wa sheria ya mazingira;

  2. Kufanya ukaguzi, ufuatiliaji na tathmini za kimazingira ili kuhakikisha utekelezaji wa Mpango wa Usimamizi wa Mazingira (EMP) na hatua za kupunguza athari, kubaini hali ya uzingatiaji wa mahitaji ya kimazingira, na kutoa taarifa kwa ngazi za juu;

  3. Kusaidia katika ukusanyaji wa sampuli na uchambuzi wake ili kubaini hali ya uzingatiaji wa viwango vilivyowekwa;

  4. Kupima na kutathmini hali ya hewa chafuzi, majitaka yanayotiririshwa, na vichafuzi vingine dhidi ya viwango vinavyoruhusiwa, na kupendekeza hatua stahiki kulingana na mahitaji ya kimazingira;

  5. Kushughulikia matukio ya kimazingira na malalamiko ya umma na kuchukua hatua stahiki;

  6. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi

Qualifications

Shahada ya kwanza katika Sayansi na Usimamizi wa Mazingira, Uhandisi wa Kemikali na Uchakataji wake, Uhandisi wa Mazingira, Uhandisi wa Mafuta na Gesi au fani nyingine inayohusiana na Mazingira kutoka katika Taasisi zinazotambulika na Serikali

Job Summary
  • Deadline: July 08, 2026
  • Positions: 19