AFISA MAHUSIANO NA MAWASILIANO II (2 Posts)

Job Description

  1. Kukusanya, kuainisha, kuchambua, kufunga na kupakia data na taarifa za mazingira kwenye tovuti na hifadhidata;

  2. Kukusanya na kushughulikia malalamiko kutoka kwa umma na kutoa mrejesho;

  3. Kuandaa taarifa kwa vyombo vya habari na matangazo ya umma kwa vyombo vya habari vya kuchapisha na vya kielektroniki;

  4. Kuendeleza programu za uhamasishaji na ufahamu wa mazingira;

  5. Kufuatilia masuala yanayojitokeza kwenye vyombo vya habari na kutoa majibu yanayofaa;

  6. Kusaidia kuratibu maandalizi na kupanga mahojiano na vyombo vya Habari;

  7. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Qualifications

Shahada ya Chuo Kikuu katika Mahusiano ya Umma, Uandishi wa Habari, Mawasiliano ya Umma, Mahusiano ya Kimataifa au Vyeti vinavyolingana kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

Job Summary
  • Deadline: July 08, 2026
  • Positions: 2